PATA MATOKEO MAZURI KWA KUFUGA SAMAKI
AINA YA KAMBALE KWA KUZINGATIA USHAURI WA KITAALAMU Godfrey, Christopher Sway Aquaculturists Sokoine University of Agriculture.
0752799673 / 0655859810.
Kambale (Claries gariepinus),
ni aina ya samaki ambao wanafugwa kwenye maji baridi na wanauwezo wa
kustahimili mazingira magumu kulinganisha na samaki wengine.Samaki hawa wapo
spicies au wanatajwa kwa majina mbalimbali kulingana na eneo na jamii husika.
Samaki hawa unaweza kusikia wakitajwa kwa majina mengine kama vile, kambale
channel, koleo, samaki kidevu, samaki wa kwenye matope. N.k. Samaki hawa
(kambale) wanakua kwa kiasi kikubwa sana kwanzia kilo 3 na kuendelea.Kambale
hawana magamba na wanauwezo wa kustahimili upungufu mkubwa wa oxygen kwenye
maji ya bwawa kwakua na mifumo miwili ya upumuaji katika mwili wao.
ASILI YA KAMBALE
Asili ya samaki hawa ni Amerika ya
Kaskazini. Samaki hawa hukua kwa haraka sana, na kuwa na uzito mkubwa. Aina hii
ya samaki hupendwa na watu wengi kwa kuwa nyama yake ina ladha nzuri na ni
laini sana. Samaki hawa huzaliana vizuri zaidi wanapokuwa mtoni au sehemu
ambayo wanapata tope. Mfugaji anapokusudia kufuga aina hii ya samaki
kibiashara, ni vyema kama ataweza kusakafia bwawa ili kuepuka uharibifu
unaoweza kusababishwa na samaki hawa. Kambale wakufugwa kwenye mabwawa
hawazaliani kabisa kwan mazingira ya ufugaji wa kwenye mabwawa sio mazuri kwao
katika kuzaliana.Hawa wanazalishwa kitaalam kwa kutumia Homone.
UMBILE LAKE
Samaki aina ya kambale wana umbo
refu, pia ni wapana kuanzia shingoni, ingawa kichwa ni kidogo, na upande wa mkia
ni mwembamba. Samaki hawa wana rangi ya kijivu na wengine nyeusi
AINA YA CHAKULA NA ULISHAJI
WA KAMBALE
Kambale ni aina ya samaki wanaokula
nyama (carnivorous) kwahio chakula chake kinahitaji kiwe na viini lishe vya
protini kwa kias kikubwa kwa ajili ya ukuaji kulinganisha na aina zingine za
viini lishe vingine kama kabohaidreti, mafuta na vitamin.Unaweza kulisha
kambale kwa kutumia unga wa samaki, maharagwe yaliyosagwa, mahindi, mchele
pumba, ngano na bidhaa nyingine. Unaweza kujenga mfumo ambao utawawezesha
samaki hawa kupata aina mbalimbali za wadudu, pamoja na majani, ili kusaidia
wapate mlo kamili.
Kambale kama aina nyingine za
samaki,wanalishwa kwa kuzingatia utaratibu maalumu kama ulishaji wa kuzingatia
uzito wake na pia ulishaji wa kuangalia uchangamkiaji na uharaka katika kula (response).
Hii inasaidia kuepusha upotevu wa chakula na uchafuzi wa bwawa pindi mabaki
mengi ya chakula yanapozama kwenye maji na kuoza ambapo inachangia uimara na
usafi wa maji kupungua.
UKUAJI NA UVUNAJI WA KAMBALE
Aina hii ya samaki, wakitunzwa
vizuri, kwa kuwapatia mazingira mazuri, chakula chenye ubora, maji safi na yakutosha wanaweza kukua kwa haraka na kuwa na
uzito mzuri unaoweza kumpatia mfugaji faida nzuri.Kambale wanaweza kufugwa kwa
wingi katika eneo dogo ukilinganisha na samaki wengine kama perege. Unaweza
kuanza kuvuna kambale baada ya miezi sita tangu walipopandikizwa kwenye bwawa.
SOKO LA KAMBALE
Jambo muhimu la kufikiria kabla ya kuanza
ufugaji wa samaki kibiashara Fikiria ni wapi utapata wateja kulingana na zao
unalozalisha (samaki) soko la samaki ni muhimu sana kutiliwa maanani kabla ya
kuanza kuzalisha.
Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.
Wafugaji walio wengi, wamekuwa wakianzisha miradi ya ufugaji wa samaki kwa kufuata mkumbo bila kutambua kwanza soko watakalozalishia samaki hao. Jambo hili huwafanya wafugaji kuwa na kipato kidogo tofauti na nguvu waliyotumia kuzalisha.
Inapofikia wakati wa kuvuna samaki,
kiasi kikubwa huuzwa papo hapo bila kufika kwenye soko halisi, jambo
linalosababisha kipato kuwa duni. Ni vyema mfugaji akawa na soko maalumu ambalo
atazalishia. Unaweza kuzalisha kwa ajili ya shule, hospitali, vyuo, au taasisi
yoyote. Halikadhalika jamii inayokuzunguka na taasisi nyinginezo.
Katika kuhakikisha mfugaji wa samaki
anapata faida kubwa ni lazima kuzingatia size ya samaki inayohitajika katika
soko husika ili kuepuka kukuza samaki kupita size ya soko ambapo itakua ni
hasara kwa mfugaji.Kiasi cha samaki wanaotakiwa kuvuliwa kwa ajili ya soko ni
lazima kizingatiwe kwa kukidhi mahitaji ya wateja waliopo. Pia ni lazima
kipindi au msimu wa kuvuna samaki kiangaliwe kwa makini mfano kuzingatia
kipindi ambacho aina ya samaki unaozalisha wanakua sio wengi sana sokoni na hii
inapelekea kutoathiri biashara yako.
HAYA YAZINGATIWE KWA UFANISI WA SOKO LA SAMAKI
- Hakikisha samaki wako katika hali ya usafi na vyombo salama unapovua tayari kwa kupeleka sokoni. Hii itapelekea kuzuia contamination na vijidudu vinavyosababisha magonjwa kama vile bacteria, fungus, na virus ambavyo pia vinasababisha samaki kuoza.
- Samaki ni bidhaa inayoharibika kwa haraka, hivyo hakikisha unawapeleka sokoni mara tu baada ya kuwavua.
- Hakikisha gharama za usafiri, utunzaji na uhifadhi, zinalipwa kutokana na bei ya soko.
- Kumbuka gharama za uhifadhi wa bidhaa inayoharibika haraka kama samaki ni kubwa, hivyo vua kwa awamu kulingana na mahitaji.
- Unaweza kuongeza thamani ya samaki kwa kufanya mambo ya msingi yanayohitajika kwenye uandaaji wa samaki, kama vile kuparua na kutumbua.
- Unaweza kuwasafisha, na pia kuwakaanga kulingana na soko husika.
- Kwa kuzingatia mambo hayo machache, mfugaji anaweza kufanya maamuzi sahihi kabla ya kuwekeza kwenye mradi wa ufugaji wa samaki. Pia ni muhimu kuzingatia mahitaji muhimu ya ufugaji wa samaki, ili kuepuka gharama zisizo za lazima.
No comments:
Post a Comment