UFUGAJI
WA KUCHANGANYA SAMAKI NA WANYAMA WENGINE (ufugaji mseto) INTEGRATED AGRO
AQUACULTURE Aquaculturist Godfrey Christopher 0752799673/0655859810
Ufugaji mseto wa samaki ni ufugaji
ambao bwawa la samaki linakuwa ndani ya shamba pamoja na shughuli nyingine za
shamba aidha hapo hapo shambani au katika eneo lililo mbali kidogo na shamba.
Shughuli za shamba zinazoenda sambamba na ufugaji wa samaki ni pamoja na kilimo
cha mazao mbalimbali kama vile mboga mboga, mpunga n.k., au ufugaji wa wanyama
mbalimbali kama vile kuku, nguruwe, ngombe, bata, mbuzi nk.
Lengo kuu hasa la Ufugaji mseto wa
samaki, wanyama na kilimo cha mazao ili kuongeza tija kwa wakulima wadogo
wadogo. Makala hii inaelezea mambo
mbalimbali ya kuzingatia kuhusiana na ufugaji huu wa samaki mseto.
FAIDA ZA UFUGAJI
SAMAKI MSETO
Kufuga samaki pamoja na shughuli
nyingine za shamba kuna faida zifuatazo:
(i) Kunaongeza ufanisi, mavuno na hatimaye faida inayopatikana inakuwa kubwa.
(ii) Kunakuwa na matumizi mazuri eneo la shamba, pembejeo pamoja na nguvu kazi.
(iii) Kunaongeza ufanisi katika kuhudumia mabwawa ya samaki kwa kuwa shughuli zote hufanyika pamoja.
(iv) Mazao ya kilimo ama mabaki yake hayapotei bali yanatumika katika kulishia samaki.

MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA KUANZISHA UFUGAJI
MSETO
Kabla ya kuanza ufugaji mseto mkulima inabidi ajiulize maswali yafuatayo:
Kabla ya kuanza ufugaji mseto mkulima inabidi ajiulize maswali yafuatayo:
(i)
Ni kiasi gani anataka kuwekeza katika mradi
(ii) Ni kiasi gani cha pesa pamoja na nguvu kazi atakavyotumia kutoa huduma kwenye mabwawa ukilinganisha na shughuli zingine za shamba?
(iii) Ni kwanini anafuga samaki? Je, ni kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa samaki kama kitoweo nyumbani au kipato au anafuga kwa sababu jirani au rafiki yake anafuga?
Katika ufugaji mseto wa wanyama na samaki, aina ya wanyama inabidi izingatie imani ya kidini katika eneo husika la ufugaji na walaji. Pia inabidi mfugaji azingatie suala la upatikanaji wa vyakula vya mifugo.

AINA ZA UFUGAJI MSETO
WA SAMAKI
Ufugaji mseto wa kilimo cha mazao na samaki
Mimea inayolimwa mashambani au isiyolimwa yaweza kutumika kama chakula cha samaki au kutengenezea chakula cha samaki. Mimea hii pia yaweza kutumika kama mbolea ya kurutubisha shamba hasa pale ambapo mbolea za wanyama ni nadra kupatikana. Mimea ambayo imekuwa ikitumika katika maeneo mengi kama chakula cha samaki ni pamoja na majani tembo, mahindi, viazi vitamu, mtama, maharage ya soya, mboga mboga kama mchicha, sukuma wiki, spinachi, chinese n.k. Mabaki ya mazao yatokanayo na mimea kama vile mihogo, maganda ya ndizi, majani ya mapapai na maganda yake, pumba za mahindi, mtama, ufuta na mpunga hutumika kama chakula cha samaki. Kama eneo linafaa kwa kilimo cha mpunga basi mkulima anaweza kutengeneza mseto wa mpunga na samaki. Kambale na Perege wanaweza kufugwa katika mashamba ya mpunga hasa msimu wa kulima mpunga. Kwenye shamba la mpunga mbolea inaweza kuongezwa ili kuongeza uzalishaji wa vyakula vya asili kwa ajili ya samaki

Mseto wa Kuku au Bata na Samaki:
Wakulima wengi huwa wanafuga kuku au bata katika maeneo yao ya kuishi. Faida au mazao yatokanayo na kuku ni pamoja na mayai, nyama na samadi ya kuku. Samadi ya kuku ina virutubisho vingi kwa matumizi ya shamba pamoja na mabwawa ya samaki. Katika mseto huu banda la kuku au bata linaweza kujengwa kando ya bwawa au juu ya bwawa la samaki. Katika mseto wa bata na samaki, huwa bata anatumia bwawa kama sehemu ya kuishi na malisho wakati huo akiwa anarutubisha bwawa. Bata huwa wakati wa mchana anatafuta chakula ndani ya bwawa na usiku anakuwa kwenye banda. Bata huwa wanakula viluwiluwi wa Chura, vimelea vya mbu, wadudu na majani ambayo yapo ndani ya bwawa.
(ii) Mseto wa Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo au Sungura na Samaki:
Tofauti na kuku au bata, mbolea itokanayo na kinyesi cha wanyama kama ng’ombe, mbuzi na kondoo huwa ina virutubisho vichache. Hata hivyo hii mbolea inaweza kutumika baada ya kuikusanya kwa muda kabla ya kuitumia. Rojorojo itokanayo na kinyesi cha ng’ombe baada ya kupitia kwenye mtambo wa biogesi ni nzuri zaidi kutumika katika mabwawa ya samaki. Mbuzi na kondoo wanaweza kutumika ingawa katika maeneo mengi ni vigumu kukusanya kinyesi chao kutokana na mfumo wa ulishaji. Kinyesi cha sungura pia kinaweza kutumika katika kurutubisha bwawa kwa kujenga banda juu ya bwawa kama ilivyo kwa upande wa ufugaji kuku.
(iii) Mseto wa Nguruwe na Samaki:
Ufugaji mseto unaweza kufanyika kwa nguruwe mdogo mwenye umri wa kuanzia mwezi mmoja na nusu hadi miezi mitatu hadi kufikia kiwango cha uuzaji yaani kilo 60 hadi 100 kwa muda wa miezi 5 hadi 6. Pia unaweza kufanyika kwa kufuga nguruwe mwenye uzito kuanzia kilo 10 hadi 15 kwa kipindi cha siku 180 ambapo atauzwa akiwa na wastani wa kilo 80 hadi 105. Kwa mseto huu mzunguko mmoja wa samaki unaenda sambamba na mzunguko mmoja wa nguruwe. Kwa maana hiyo kwa muda wa miezi sita (6) mfugaji anavuna nguruwe na samaki kwa wakati mmoja. Idadi ya wanyama inatakiwa iendane na mahitaji ya mbolea kwenye bwawa. Kwa kawaida wanahitajika nguruwe 60 kwenye bwawa lenye ukubwa wa hekta moja. Nguruwe mmoja ana uwezo wa kutoa mbolea kwa wastani wa kiasi cha kilo 6.5 hadi 7.5 kwa siku.
AINA YA SAMAKI WANAOFAA KATIKA KILIMO MSETO
Perege na Kambale ni samaki wanaofugwa katika maeneo mabalimbali hapa Tanzania. Perege ndiye ambaye anafahamika zaidi kwa wafugaji. Chakula cha asili cha Perege ni vimelea vya kijani vilivyomo ndani ya maji, lakini ana uwezo wa kula aina nyingi za vyakula ikiwa ni pamoja na pumba za mahindi na mpunga, majani na mabaki ya jikoni. Vile vile anakua vizuri kama kutakuwa na mbolea za samadi na za chumvi chumvi, na anaweza kuhimili kiasi kidogo cha hewa ya oksijeni. Madume ya Perege hukua haraka zaidi kuliko majike, na uvunaji unaweza kufanyika baada ya kufikisha uzito wa gramu 250. Kambale hula vyakula vya asili ndani ya maji kama vile wadudu, konokono, vifaranga wa chura na samaki wengine wadogo. Vile vile anakula vyakula vya ziada kama vile mabaki ya vyakula hasa yenye asili ya nyama. Kambale hutumika kupunguza wingi wa Perege ndani ya bwawa. Hii ni kutokana na ukweli kwamba Perege anazaliana kwa wingi kwenye bwawa. Kambale anakua haraka sana kama chakula chenye protini kinapatikana kwa wingi. Kambale anaweza kuishi kwenye maji yenye hewa kidogo ya oksijeni. Tofauti na Perege, Kambale ana mifupa michache na minofu mingi na ni mtamu hasa anapokaushwa kwa moshi.
FAIDA ZA MBOGA MBOGA KATIKA UFUGAJI
MSETO
(i) Chanzo cha chakula cha samaki. Mboga mboga hutumika moja kwa moja kama chakula cha samaki kwa kuwa jamii ya samaki wengi wanaofugwa ni wale wanao kula majani kama jamii ya Sato na Perege na hata jamii ya Kambale. Hivyo mabaki ya mboga mboga kutoka bustani hukatwa katwa vipande vidogo vidogo kwa ajili ya kulisha samaki.

(ii) Chakula cha mkulima. Hili huwa lengo kuu la kulima mboga mboga kwenye mseto na ufugaji samaki. Chakula jamii ya mimea huwa na kiwango kikubwa cha madini yanayohitajika katika utunzaji wa afya ya mwanadamu. Hinyo mboga mboga hupunguza gharama ya ununuzi wa chakula kwa mkulima kwa kumwezesha mkulima kupata lishe bora kutoka shambani kwake.
(iii) Chanzo cha fedha. Ufugaji mseto wa samaki na bustani hulenga kuwa kitega uchumi kikubwa kwa wakulima wadogo. Mavuno ya mazao ya bustani huuzwa kirahisi kwa kuwa yanahitajika kwa wingi na jamii kutokana na umuhimu wake. Fedha inayopatikana husaidia katika utunzaji wa shamba mseto ama kutumika katika mahitaji mengine ndani ya familia ya mfugaji.
(iv) Mbolea kwenye bwawa la samaki. Mboga mboga hutumika kama mbolea kwenye bwawa la samaki. Mboga mboga huozeshwa kwenye hori ili iwe mboji ambayo hutoa mimea na wadudu wa asili ambao hutumika kama chakula cha samaki. Hii hupunguza gharama za uzalishaji kwenye bwawa la samaki.
FAIDA ZA KUKU KATIKA UFUGAJI MSETO
(i) Chanzo cha mbolea. Lengo kuu la ufugaji wa kuku kwenye ufugaji mseto ni urutubishaji wa bwawa la samaki ili kupata chakula cha asili kwa samaki. Kinyesi cha kuku hutumika kama chanzo cha mbolea kwa sababu huwa kina kiasi kikubwa cha urea.
(ii) Hutoa chakula cha samaki. Tofauti na kuwa chanzo cha rutuba, kinyesi cha kuku huliwa moja kwa moja na samaki. Hiki huwapa samaki afya nzuri kwani huwa na chembechembe nyingi za urea ambazo ni sehemu kubwa ya madini ya Nitrojeni na Fosforasi ambayo huhitajika kwa wingi kwenye chakula cha samaki.
(iii) Chanzo cha chakula kwa wafugaji. Pamoja na kuwa na umuhimu wa kiikolojia katika ufugaji mseto, lengo jingine kubwa ni kuwa chanzo cha lishe bora kwa mfugaji kwani huwa na protini ya kutosha ambayo husaidia katika ukuaji wa mwili.
(iv) Chanzo cha fedha. Kama ilivyo kwa mifugo wengine, mauzo yatokanayo na mazao kama kuku husaidia kama chanzo kikubwa cha fedha kuanzia wafugaji wadogo wadogo hadi wakubwa. Kuku hufugwa kirahisi kulinganisha na wanyama wakubwa kama vile ng’ombe, nguruwe, mbuzi na kondoo ambao huhitaji eneo kubwa, rasilimali kubwa, wasimamizi wengi, n.k. Hivyo ufugaji wa kuku huwa na gharama ndogo kiuendeshaji na huleta faida kubwa.
www.fishfarmingskills.blogspot.com
gsway32@gmail.com
contact: 0752799673/ 0655859810
gsway32@gmail.com
contact: 0752799673/ 0655859810
No comments:
Post a Comment