Monday, 26 March 2018

UFUGAJI SAMAKI AINA YA PEREGE


ONGEZA KIPATO CHAKO MARADUFU KWA KUFUGA SAMAKI AINA YA PEREGE 
Ufugaji samaki ni kazi ya kupanda, kukuza na kutunza samaki katika mabwawa, mito, mifereji au eneo lililotengwa kwa ajili ya ukusanyaji wa maji, (water harvesting ponds) uzio (uliotengenezwa kwa vyuma, nyavu 
au miti) au eneo lolote ambalo udhibiti wake yako chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe. Mabwawa  ya samaki hutengenezwa au huchimbwa kwa njia tofauti tofauti, yaweza kuwa ni ya 
kuchimbwa na watu (japokuwa ya asili pia huweza kutumika) Samaki pia wanaweza kufugwa baharini au ziwani kwa kutumia vizimba (cages) Pia uzio unaweza kuwekwa katika eneo lolote lililo na maji kama ziwa au baharí au chemichemi. Perege /sato /Tilapia wapo wa aina tofauti tofauti kama vile perege wa Mosambique, Perege weusi, perege wa victoria na wale shiranus. Tofauti zao ni ndogo sana na mara nyingi ni vigumu kuwatambua.
Ufugaji samaki kwa kiasi fulani si sawa na ukuaji samaki katika mito, maziwa na bahari. Tofauti iko katika huduma inayotolewa kwa samaki wafugwao na idadi ya samaki wanaopaswa kuwamo ndani ya eneo husika. Samaki waliofugwa huhitaji kulishwa na kuhudumiwa.
Ufugaji wa samaki ni sector inayokua kwa kiasi fulani licha ya changamoto zinazo ikabithi sector hii hapa Tanzania. Baadhi ya Watanzania wamekuwa wakifuga samaki katika mabwawa 
hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru. Lakini baadhi ya wafugaji wamekuwa wakitoa matunzo hafifu kwa kutofahamu vizuri mambo ya kuzingatia katika swala zima la ufugaji wa samaki kiasi cha kufanya mavuno kutokua mazuri na kupelekea sector hii kushuka na kukua kwa kusua sua. Kwa miaka ya karibuni, serikali imetilia mkazo utoaji elimu (ugani) wa ufugaji samaki ili 
kuboresha mafanikio yake. Wasomaji wetu wa makala hii watasaidika kuogeza uelewa zaidi kwenye ufugaji wa samaki.

                           MWONEKANO WA PEREGE NA UMBILE LAKE
 

Faida za ufugaji samaki
Hizi ni baathi ya faida za ufugaji wa samaki (perege)
1.  Chakula bora chenye uto-mwili (protini) muhimu inayohitajika kujenga mwili.
2.  Kujipatia kipato baada ya kuuza samaki waliofugwa.
3.  Kuboresha kazi nyingine za kilimo kama bustani ya mboga, ufugaji wa ng’ombe, bata, kuku, nguruwe, bustani ya miti, n.k.
4.  Huwezesha kutumia rasilimali ambayo isingekuwa ikitumika kama kusingekuwa na ufugaji samaki kama vile eneo la ardhi lenye maji maji, pumba za mahindi na mpunga, na mabaki ya mboga mboga kutoka bustanini kwa kulishia samaki.
5.  Eneo la bwawa huwa ni sehemu nzuri ya mapumziko.
6. Perege pia wanasoko kubwa hapa Tanzania kwan wanakubalika na watu wote.
  
Hatua muhimu  kuzingatia katika shughuli za ufugaji samaki
1.     Uchaguzi wa mahala panapofaa kwa ajili ya kuchimba bwawa la samaki.
2.     Tathmini ya umbo na ukubwa wa bwawa
3.     Uchimbaji wa bwawa.
4.     Uingizaji na utoaji wa maji katika bwawa.
5.     Uwekaji wa mbolea na (majivu).
6.     Upandaji wa vifaranga vya samaki.
7.     Ulishaji wa samaki na matunzo mengine bwawani.
8.     Uvunaji wa samaki na aina ya nyavu/zana zifaazo kutumika.
9.     Uhifadhi wa mbegu kwa ajili ya mzungoko mwingine wa upandaji samaki bwawani.

Vigezo muhimu katika kuboresha uzalishaji 
Joto au ubaridi wa maji katika sehemu husika huweza kuongeza au kupunguza hamu ya ulaji wa samaki na hivyo ukuaji wake. 
  • Chakula cha samaki (cha asili na cha ziada), aina ya chakula na kiasi kinachopatikana. Chakula cha asili ni kama vile planktonik au majani na algae wanaoota kwenye mabwawa.
  • Uwingi wa samaki waliomo bwawani kulinganisha na ukubwa wa bwawa. Hapa lazima wingi wa samaki uendane na ukubwa wa bwawa lenyewe.
  • Ubora wa vifaranga (quality) waliopandwa. Vifaranga wenye ubora mzuri huwa na uwezo wa kukua haraka.Na hapa pia mkulima anaweza kuamua kuchagua mbegu nzuri za jinsia moja (mono sex) au mchanganykio wa jinsia kwa ajili ya kupata mbegu za mzunguko mwingine.                                                                                                                                            www.fishfarming.blogspot.com   Phone 0752799673/ 0655859810.

3 comments:

  1. What is the casino? - SEPT
    The best casino online is the deccasino One filmfileeurope.com of the main reasons why people are spending 1등 사이트 money on a ford escape titanium game is by having a septcasino few options. One of the reasons

    ReplyDelete