NJIA KUU ZA KUZINGATIA
WAKATI WA KUANZISHA
UFUGAJI WA SAMAKI
• Mfugaji
anatakiwa awe na shauku na dhamira ya kweli ya ufugaji.
• Kufanya
tathmini ya rasilimali alizonazo kwa ajili ya mradi wa ufugaji wa samaki.
• Chanzo
endelevu cha mtaji kwa ajili ya mradi.
• Hulka
ya uvumilivu na kuthubutu.
• Tathmini
ya soko la bidhaa za samaki.
• kujipatia
maarifa ya msingi ya ufugaji wa samaki
SIFA ZA
ENEO LA KUFUGIA SAMAKI
· Eneo
la kufugia samaki linatakiwa liwe na maji ya kutosha kwa mwaka mzima.
· Eneo
la kufugia samaki linatakiwa liwe na udongo unaoweza kutuamisha maji.
· Eneo zuri la kufugia samaki ni kuwa eneo lisiwe na
historia ya mafuriko, kwa kuwa mafuriko yakitokea samaki waliokuwa bwawani
wataondoka na maji na bwawa litafunikwa na udongo.
· Eneo zuri la kufugia samaki ni lile
linalofikika kwa urahisi.
· Eneo la kufugia samaki pia linatakiwa kuwa ni eneo lenye
amani na utulivu na watu wenye kuelewana.
· Kuwa na soko la bidhaa.
· kuwa na umiliki wa ardhi wa uhakika.
AINA
NA JINSI YA UTENGENEZAJI WA BWAWA LA SAMAKI
Zipo
namna mbalimbali za utengenezaji wa bwawa la samaki, kulingana na aina ya bwawa
lenyewe, Hali ya uchumi, wingi wa samaki watakaofugwa pamoja na aina ya samaki
watakaofugwa.
Zifuatazo ni Aina za mabwawa ya kufugia samaki.
1.Bwawa la kuchimba udongo bila kujengea
"Earthen Pond.
2. Bwawa la kuchimba udongo na kujengea kwa
Matofali, Simenti na
Zege.
JINSI YA KUANDAA NA
KUPANDIKIZA VIFARANGA AU MBEGU ZA SAMAKI KATIKA BWAWA LAKO.
Kabla ya kuvisafirisha
vifaranga kutoka kwenye bwawa wanaloishi ni vema vikatolewa na kuwekwa kwenye
vibwawa vidogo vidogo kwa muda wa kati ya saa 24 hadi 72 (kutegemeana na umbali
wa safari) bila chakula.
Wakati wa kupandikiza
mfugaji anatakiwa akifika asivimwage vifaranga kwenye bwawa bali anatakiwa
kuyaruhusu maji yaliyobeba vifaranga yabadilishane ujoto na maji yatakayopokea
vifaranga. Hapa mfugaji anatakiwa kuliweka kontena au chombo alichobebea
vifaranga kielee kwenye maji anayotaka kufugia kwa muda wa dakika kati ya 30
hadi 35, baada ya hapo chombo kilicho na vifaranga kifunguliwe na kiinamishwe
ili maji hayo yaweze kukutana na yale yaliyoandaliwa kwa ajili ya kufugia na
hapo ataruhusu vifaranga kuingia wenyewe kwenye bwawa husika.
Iwapo utafika na kuvimwaga
vifaranga kwenye bwawa jipya bila kufuata utaratibu huo wa kitaalamu basi
tofauti ya ujoto wa maji kati ya chombo kilichosafirishiwa vifaranga na bwawa
unaweza kusababisha vifaranga wote kufa kwa muda mfupi, kitaalamu wanasema kuwa
vifo vya vifaranga hivyo vinasababishwa na mshituko wa joto.
Jambo lingine la
kuzingatia ni kuwa uandaaji na usafirishaji wa vifaranga ni vizuri ukafanywa
muda ambao hali ya hewa inakuwa na ubaridi. Muda unaopendekezwa zaidi na
wataalamu ni asubuhi au jioni kwa sababu muda huo samaki wanakuwa na uwezo wa
kuhimili misukosuko ya safari tofauti na hali ya hewa inapokuwa ya joto.
UFUGAJI WA SAMAKI WAKATI
WA KIANGAZI NA MASIKA
Kimsingi hakuna tofauti
kubwa wala athari kubwa sana za ufugaji wa samaki wakati wa kiangazi
ukilinganisha na wakati wa masika, tofauti zilizopo ni ndogo ndogo ambazo
kitaalamu hazina madhara makubwa kwa mfugaji.
Ø ulaji wa chakula wa samaki na ukuaji wao
Ø uchafuzi
wa maji yanayoingia kwenye mabwawa ya kufugia
ULISHAJI NA
UTUNZAJI WA SAMAKI BWAWANI.
• Samaki
wapewe chakula angalau mara 2 kwa siku (saa 3-4 asubuhi na
9-10 jioni) /hewa ya kutosha .
• Kuwapa
vyakula tofauti kutegemeana na silka ya aina ya samaki unaowafuga.
• Kuna
samaki wanaofaidika na vyakula vya nyama nyama kama vile kambale na sangara
(hawa hawali pumba) na kuna samaki wengine kama sato wanakula vyakula
mchanganyiko wa nyama na mboga mboga na wapo wengine wanaokula vyakula vyenye
asili ya mimea tu “carps”.
TABIA ZA ULAJI WA SAMAKI
1) Samaki
wanaokula nyama, (sangara na kambale).
2) Samaki
wanaokula mimea ‘carps’.
3) Samaki
wanaokula vyakula mchanganyiko (nyama na mimea) kama perege, sato na mwatiko
(samaki wa maji chumvi).
Wanga 20-25%
Mafuta 10-15%
Vitamin 1-2%
Madini 1-2%
Protini 18-45%
NB; Maji – hapa ifahamike kuwa wakati
tunazungumzia viwango vya maji vinavyohitajika kwa wanyama wengine wafugwao,
hitaji la maji kwa samaki ni ubora wa maji anayofugiwa na sio wingi wake.
TARATIBU ZA
ULISHAJI WA SAMAKI
MASOKO YA SAMAKI
Ø Soko
la awali, hili ni soko la moja kwa
moja kutoka kwa muuzaji ambaye ni mfugaji kwenda kwa mlaji,
Ø Soko
la kati, katika soko hili kwa
kawaida kunakuwa na mtu wa kati ambaye ananunua samaki kwa mfugaji kwa lengo la
kwenda kuwauzia walaji.
Ø Soko
la kimataifa, hili ni soko
linalofanyika nje ya nchi (baina ya nchi moja na nchi nyingine).
Kwa mawasiliano tutafte kupitia www.fishfarmingskills.blogspot.com gsway32@gmail.com
Kwa mawasiliano tutafte kupitia www.fishfarmingskills.blogspot.com gsway32@gmail.com
contact. 0752799673/ 0655859810
Facebook jina ni Gody sway
Gudgud
ReplyDelete